TUNAZOTOA HUDUMA YA KUANDIKA BARUA YA MAOMBI YA KAZI KWA KIINGEREZA

l

KUANDIKA CV

Waandishi wetu watakuadikia CV kulingana na vigezo vya eleimu na elimu yako, CV yako itawekwa katika mpangilo sahihi unaofaa kwa waajiri, unachohitaji ni kutuma maelezo yako binafsi

h

BARUA YA MAOMBI

Barua ya maombi ni kitu muhim sana katika uombaji wa kazi, barua yenye Lugha na mpangilio mzuri husaidia sana kupunguza maswali wakati wa interview. Team yetu itakusaidia kuandika barua yenye mvuto kwa waajiri.

KU-EDIT CV YAKO

Je uko na CV lakini huna uhakika na mpangilio wa maelezo yako? basi tutakusaidia ku-edit na kuweka katia mpangilio unaofaa kwa waajiri

JINSI YA KUANDIKA BARUA YA MAOMBI YA KAZI KWA KISWAHILI

Barua ya maombi ya kazi huandikwa kwa malengo ya kuomba kazi. Kujifunza namna sahihi ya uandishi wa barua ya maombi ya kazi si kwamba utakusaidia katika kujibu maswali pekee, bali ujuzi huu utakufanya upate kazi halisi wakati utakapo hitaji kufanya hivyo.

Nakumbuka niliwahi kuitwa kufanya kazi katika kampuni ya global publishers kwa sababu tu, niliandika vyema barua yangu ya maombi ya kazi.

MUUNDO WA BARUA YA MAOMBI YA KAZI
i.             Anuani ya mwandishi. Yaani anuani yako wewe unayeandika barua hiyo.
ii.            Tarehe.
iii.           Anuani ya anayeandikiwa.
iv.          Salamu.
v.           Kichwa cha habari.
vi.          Kiini cha barua. Hii ni roho ya barua yako, ukikosea mahali hapa, kama unajibu swali katika mtihani, utapoteza alama. Na kama unaomba kazi halisi, utaikosa. Kiini kina aya nne:
–      Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo. Ni katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.

–      Katika aya ya pili, eleza ujuzi wako kwa ufupi. Usieleze sana. Barua hii haipaswi kuwa ndefu kupindukia.

–      Aya ya tatu eleza kwa nini upewe kazi hii wewe na si mtu mwingine. Epuka kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi. Maneno kama, ninaomba kazi hii ili niweze kumtibia mama yangu mgonjwa kitandani, hayana msaada.
–      Aya ya nne eleza uko tayari kwa usahili siku gani?
vii.         Mwisho wa barua. Mwisho wa barua yako uwe na:
–      Neno la kufungia. Wako mtiifu. Wako katika ujenzi wa taifa n.k
–      Sahihi yako.
–      Jina lako

Are you looking for Job oportuninty?

 

SIGN UP FOR JOB ALERT!

We'll send new, local jobs straight to your inbox
Enter your e-mail and subscribe to our newsletter.